Search This Blog

Thursday, March 5, 2020

Ubora Yanga, Simba uko hapa Jumapili

By Charles Abel

Dar es Salaam. Viungo wa Yanga na safu ya ulinzi ya Simba wana nafasi kubwa ya kuamua mchezo baina ya timu hizo utakaochezwa Jumapili, Machi 8 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kila timu ina kibarua cha kuhakikisha unadhibiti idara inayoonekana kuwa na nguvu na uimara ambao huchangia ipate matokeo mazuri katika mechi zao.

Yanga ambayo itakuwa mwenyeji wa mchezo huo, safu yao ya kiungo inapaswa kuhakikisha inaizima ile ya Simba ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kupata ushindi katika mechi hiyo.

Safu ya kiungo ya Simba imekuwa uti wa mgongo wa kuzalisha na kufunga mabao tofauti na ile ya Yanga.

Katika jumla ya mabao 55 ambayo Simba imefunga, 18 yamefungwa na wachezaji sita wanaocheza safu ya kiungo.

Wachezaji hao ni Hassan Dilunga aliyepachika sita, Francis Kahata (4), Gerson Fraga (3), Clatous Chama na Jonas Mkude waliofunga mawili kila mmoja wakati Sharaf Shiboub amepachika bao moja.

Advertisement

Mfumo wa kujaza idadi kubwa ya wachezaji katika safu ya kiungo imekuwa chachu ya Simba kupata ushindi na idadi ya kutosha ya mabao msimu huu kutokana na uwezo wao wa kutengeneza nafasi na kufunga.

Hali iko tofauti kwa Yanga ambayo safu ya kiungo imekuwa haina ubora wa hali ya juu hasa katika kujenga mashambulizi na kufunga na kudhihirisha hilo, viungo wa Yanga wamefunga mabao manne tu kati ya 29 ambayo timu hiyo imepachika hadi sasa.

Mapinduzi Balama mwenye mabao mawili, Haruna Niyonzima na Abdulaziz Makame ambao kila moja amepachika bao moja ndio viungo pekee wa Yanga waliofunga.

Pamoja na Yanga kuonekana kuwa butu katika kutumia nafasi, bado wanaitegemea zaidi safu ya ushambuliaji ambayo imefunga mabao 25 kati ya 29 ambayo timu hiyo imefunga katika Ligi Kuu hadi sasa.

Kinara wa ufungaji Yanga katika safu ya ushambuliaji ni David Molinga mwenye mabao manane akifuatiwa na Patrick Sibomana (3).

Ditram Nchimbi, Benard Morrison, Juma Balinya ambaye ameondoka, Tariq Seif na Mrisho Ngassa, Yikpe Gnamien kila mmoja amefunga mabao mawili na moja Sadney Urikhobi (ameondoka).

Hata hivyo safu ya ushambuliaji ya Simba nayo ni tishio na inapaswa kuwafanya walinzi wa Yanga kucheza kwa umakini muda wote wa mchezo.

Washambuliaji wa Simba wamefunga mabao 32 kati ya 55 ambayo timu hiyo imepachika hadi sasa ambapo kinara wao ni Meddie Kagere ambaye amefumania nyavu mara 15 akifuatiwa na Miraji Athumani mwenye sita.

Deo Kanda ana mabao matano wakati John Bocco na Luis Miquissone wana matatu huku Ibrahim Ajibu akiwa na bao moja.

Kocha Kennedy Mwaisabula alisema Simba itabebwa na viungo katika mchezo huo kwa kuwa wachezaji wa eneo hilo ni wazuri wakati Yanga kama mawinga wao watakuwa vizuri basi mechi itakuwa kali.

“Simba ina viungo wazuri wanaochangamsha mpira na wanahamasisha kuwatazama hivyo hata katika mchezo huo watakuwa vizuri katika eneo hilo.

“Yanga inatumia mawinga wakiongozwa na Morrison, pia viungo kama Haruna Niyonzima, Mohammed Banka, Balama Mapinduzi na Fei Toto wakiwa katika ubora wao itakuwa vita kubwa katikati ya uwanjani,”alisema.

Mchambuzi Ally Mayay alisema kitu kitakachoibeba Simba ni hali ya upambanaji ya wachezaji wote uwanjani bila kujali wanacheza nafasi gani.

“Aina ya mchezo ambao Simba wanacheza inawafanya timu nzima kuwa vizuri hata kama wana viungo wazuri lakini huwa wanacheza total football ndio maana kuna kipindi kocha wao alijaribu kuanza kumtumia mshambuliaji mmoja lakini akaona hampi matokeo mazuri ikabidi awe anatumia washambuliaji wawili Kagere na Bocco.

“Yanga nguvu yao kubwa iko pembeni ambako wanatumia zaidi mawinga wakiongozwa na Benard Morrison hivyo hata katika mchezo huo wanaweza kuendelea kutumia mfumo huo na ukawapa matokeo,”alisema Mayay ambaye alikuwa mchezaji wa kutumainiwa Yanga na Taifa Stars.

Let's block ads! (Why?)

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...