Search This Blog

Sunday, March 1, 2020

Samatta amchongea beki wa Manchester City

London, England. Mbwana Samatta wa Aston Villa amemponza beki wa kati Manchester City Jones Stones.

Idadi kubwa ya mashabiki wa Man City wamemtaka kocha Pep Guardiola kumuacha Stones kutokana na makosa ya mara kwa mara.

Stones jana alifanya kosa lililompa nafasi Samatta kufunga bao kwa mpira wa kichwa baada ya kuteleza.

Beki huyo wa England aliteleza na kumpa nafasi winga Anwar El Ghazi kupiga krosi iliyotua kichwani kwa Samatta.

Licha ya Man City kutwaa Kombe la Ligi kwa ushindi wa mabao 2-1, mashabiki wa klabu hiyo waliandika katika mitandao yao wakitaka Stones auzwe.

Baadhi ya mashabiki walimfananisha Stones na beki Phil Jones wa Manchester United ambaye amekuwa akifanya makosa mara kwa mara.

Advertisement

“John Stones hatumtaki Man City msimu ujao, aina ya uchezaji wake kama Phil Jones,”aliandika mmoja wa mashabiki.

Pia wengine walisema aina ya makosa anayofanya Stones ni sawa na yale ya beki wa Liverpool Dejan Lovren. 'John Stones has gotta seriously go, City’s equivalent of Lovren.

Let's block ads! (Why?)

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...