
LONDON, ENGLAND. RIO Ferdinand amesema hana mashaka kwamba Jose Mourinho atafanya kila analoweza kumzuia straika wake Harry Kane kuihama Tottenham Hotspur na wkennda kujiunga na Manchester United.
Beki huyo wa zamani wa Mashetani Wekundu, Ferdinand, alisema anaamini Spurs wanapambana kwa nguvu zote kuhakikisha mshambuliaji wao huyo haondoki kwenye kipindi cha usajili cha dirisha lijalo la majira ya kiangazi.
Hakuna ubishi, msimu huu Spurs itamaliza bila ya kuwa na taji lolote na jambo hilo linazidi kuchochea kwamba litamsukuma Kane kuelekea mlango wa kutokea kwenye timu hiyo. Hilo linakuja katika kipindi hiki ambacho Man United wapo sokoni kusaka straika mpya wa kwenda kuifanya fowadi yao kuwa na makali zaidi. Lakini, Rio anaamini hata kama klabu yake hiyo ya zamani itaweka pesa nyingi mezani kumtaka Kane, Spurs hawatakuwa wepesi kumruhusu kwenda Old Trafford.
Akizungumza kupitia Instagram, Ferdinand alisema: "Ningemchukua Harry Kane kwa sasa? Bila shaka ningeweza kufanya hivyo. Kama yupo fiti na anantaka kuondoka, unaona kabisa Kane anakwenda kuwa mtu sahihi Man United, tena kwa asilimia . Mchezaji wa kiwango cha juu annayekupa uhakika wa mabao, kwenye Ligi Kuu England unakuwa na uhakika wa mabao.
"Huyu mtu anafunnga sana mabao, lakinni sioni kama Spurs wanamruhusu Kanne aondoke. Na hasa kipindi hiki ambacho Mourinho yupo kwenye timu hiyo, hawezi kumruhusu kwenda Man United.”
Staa wa zamani wa Ligi Kuu England, Alan Shearer yeye anaamini kwamba Kane hataendelea kubaki kama Spurs haitakuwa imebeba taji lolote msimu ujao.
No comments:
Post a Comment