Search This Blog

Friday, March 20, 2020

Pauni 50 milioni kumshusha Aubameyang Old Trafford

Manchester, England . WAKATI virusi vya corona vikiendelea kutikisa duniani, huku pembeni Manchester United wanafanya mambo yao kimya kimya na sasa wameanza harakati za kuivamia Arsenal.
Habari mpya kutoka korido za Old Trafford ni kwamba, mabosi wa Mashetani Wekundu hao wameingia msituni kusaka saini ya mshambuliaji na nahodha wa Arsenal, Pierre-Emerick Aubameyang.
Imeelezwa kuwa Man United imeweka mezani pauni 50 milioni kwa ajili ya saini ya straika huyo wa kimataifa wa Gabon, ambaye mkataba wake unafikia tamati mwakani.
Hata hivyo, kinachowapa uhakika Man United kumnasa Aubameyang ni baada ya kugoma kusaini mkataba mpya hivyo, hakuna namna ni lazima Arsenal wamuweke sokoni mwishoni mwa msimu huu ili kuepuka hasara.
Aubameyang aliyeifungua Arsenal mabao 20 kwenye mashindano yote msimu huu, pia anawaniwa na Barcelona huku kiu yake ikiwa ni kukipiga Real Madrid ama PSG ambazo zote hazinyaonyesha nia ya kumhitaji.
Kwa sasa Manchester United bado wanasaka mrithi sahihi wa kuziba nafasi ya Romelu Lukaku, ambaye ametimkia zake Inter Milan huku wakiwa na majanga ya Marcus Rashford na Anthony Martial ambao wote ni majeruhi.
Bosi wa Arsenal Raul Sanllehi na Mkurugenzi wa Ufundi, Edu wanted wote wanataka kuona Aubameyang akisaini mkataba mpya ili kubaki klabuni hapo kwa muda mrefu.
Hata hivyo, Sanllehi na Mkurugenzi Mtendaji wake Vinai Venkatesham, wamesisitiza kuwa hawataki kuona kilichotokea kwa Aaron Ramsey na Jack Wilshere ambao wote waliondoka wakiwa wachezaji huru, hakitokei tena kwa mchezaji mwingine.
Mbali na Auba, wengine Mesut Ozil, Bukayo Saka, Shkodran Mustafi na Reiss Nelson wote watamaliza mikataba yao mwaka 2021, lakini ishu ya nahodha huyo imekuwa ikiwapasua zaidi Arsenal.

Let's block ads! (Why?)

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...