Search This Blog
Thursday, March 26, 2020
Papa Francis amepimwa virusi vya corona
Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis amepimwa virusi vya corona (covid-19) na kuthibitika kuwa hajaambukizwa.
Papa Francis alipimwa virusi hivyo baada ya mmoja wa wachungaji anayeishi katika katika makazi yake kugundulika kuwa na corona.
Vyombo vya habari nchini Italia viliripoti kuwa mchungaji huyo ambaye ni ofisa wa sekretarieti ya jimbo aligundulika kuwa na virusi vya corona na kuzua hofu kuwa huenda Papa Francis naye ameambukizwa.
Kwa mujibu wa tovuti rasmi ya Vatican, mchungaji huyo alikuwa mmoja wa washiriki wa karibu wa papa na sasa amelazwa katika Hospitalini ya Roma wakati idadi ya walioambukizwa katika jimbo hilo ikifikia watano.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment