Search This Blog

Wednesday, March 4, 2020

Nyota Tottenham amvaa shabiki jukwaani

London, England. Kiungo wa kimataifa wa England Eric Dier jana aliruka uzio kwenda jukwaani kutaka kuzichapa na shabiki.

Tukio hilo lilitokea katika mchezo wa mashindano ya Kombe la FA ambao  Tottenham Hotspurs ilitupwa nje kwa kufungwa mabao 3-2 kwa penalti baada ya kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Norwich City.

Kocha wa Spurs Jose Mourinho alisema kiungo huyo alitolewa lugha kali na shabiki.

Dier alikwenda kwa kasi jukwaani kwenda kumvaa shabiki huyo kabla ya maofisa usalama kumzuia.

“Nadhani Eric amefanya jambo ambalo kwa mchezaji wa kimataifa hawezi kutenda, lakini kila mmoja anaweza kufanya,”alisema Mourinho.

Dier aliyecheza mechi 40 za England alishindwa kuisaidia Spurs kusonga mbele katika mashindano hayo baada ya kipa wa Norwich Tim Krul kuokoa panalti mbili.

Advertisement

Norwich inashika mkia katika msimamo wa Ligi Kuu England na matokeo hayo yamewachukiza mashabiki wa Spurs.

“Narudia kusema mchezaji wa kimataifa hapaswi kufanya, lakini narudi jambo hili linaweza kufanywa na yeyote,”alisisitiza Mourinho.

Alisema lugha ya maudhi iliyotolewa na shabiki huyo ilikuwa ya kumchukiza mchezaji huyo kwa kuwa familia yake ilikuwa uwanjani.

Katika mechi nyingine, Leicester City iliichapa Birmingham bao 1-0, pia Manchester City iliilaza Sheffield Wednesday.

Let's block ads! (Why?)

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...