Search This Blog

Tuesday, March 31, 2020

Minziro ndio basi tena Alliance FC

UONGOZI wa Alliance FC umefanya mabadiliko ya benchi la ufundi kwa kumrejesha Kessy Mzirai kuwa kocha mkuu huku Fred Felix Minziro akipangiwa majukumu mengine.

Mapema msimu huu, timu hiyo ilianza kazi na Athuman Bilali ‘Billo’ ambaye hakudumu kufuatia matokeo ya mchezo mmoja dhidi ya Mbao FC uliomalizika kwa sare ya bao 1-1.

Baada ya kuondoka Billo, majukumu yalibaki kwa Mzirai akisaidiana na Habibu Kondo ambaye kwasasa ni kocha msaidizi KMC na baadaye Minziro pamoja na Mathias Wandiba wakachukuwa nafasi huku Mzirai akijiengua.

Minziro akiwa Kocha Mkuu, amesimamia michezo 15 ikiwamo miwili ya Kombe la Shirikisho na ameshinda minne, sare nne na kupoteza saba na kuiweka timu nafasi ya 18 kwa pointi 29 kwenye msimamo wa Ligi Kuu.

Ofisa Habari wa Klabu hiyo, Jackson Mwafulango alisema Minziro hajafukuzwa isipokuwa kilichofanyika ni mabadiliko kwenye benchi la ufundi kwa lengo la kuboresha timu hasa kipindi hiki ligi imesimama.

Alisema Minziro atapangiwa majukumu mengine kutokana na klabu hiyo kuwa na timu nyingi, huku aliyekuwa Msaidizi wake, Wandiba akipewa kikosi cha Vijana (U-20).

Advertisement

“Mzirai tumemrudisha kuwa Kocha Mkuu, akisaidiwa na Gilbert Dady na Minziro atapangiwa majukumu mengine na Wandiba amepewa timu ya vijana, lengo ni kuboresha” alisema Mwafulango.

Kwa upande wa Minziro alisema hajapata taarifa zozote za aidha kusimamishwa au kupangiwa majukumu mengine, hivyo atakapopata rasmi ndio ataweza kuzungumza.

Hata hivyo, licha ya uongozi kutoweka wazi kuachana na Minziro, habari kutoka ndani ya klabu hiyo zinasema kuwa Minziro hana tena nafasi ya kuifundisha Alliance kwa maana ya kwamba ametupiwa virago.

Let's block ads! (Why?)

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...