Mara baada ya mvua kubwa kulisomba daraja la kiyegeya barabara ya Morogoro-Dodoma Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Nchi (TANROADS), Patrick Mfugale amesema barabara hiyo ni chakavu.
Ametoa kauli hiyo siku moja baada ya Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa kumuondoa katika nafasi yake Meneja wa TANROADS-Morogoro kwa madai ya kutokagua miundombinu na hivyo daraja hilo lililopo Kilosa kusombwa na maji.
Mfugale, ambaye ni mtaalamu wa Ujenzi amesema barabara hiyo ilijengwa miaka 40 iliyopita na hivyo imeshatumika muda mrefu ndio maana kila mara wamekuwa wakiifanyia ukarabati.
Amesema kuwa kukatika kwa daraja hilo ni kutokanan na uchakavu wa daraja na kwamba ni jambo la kawaida ambapo amesema kuwa kitaalamu uhai wa makalavati yanayowekwa si zaidi ya miaka 25 na kuwa tayari Serikali iko katika mchakato wa kuijenga upya barabara hiyo na madaraja yake.
Search This Blog
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment