Search This Blog

Wednesday, March 11, 2020

Mechi sita kuamua hatima ya Mbao

By Saddam Sadick

Mwanza. Baada ya kupoteza mechi yake dhidi ya Mbeya City juzi ikiwa ni mchezo wa nne mfululizo kupoteza ugenini, matumaini ya Mbao FC kubaki Ligi Kuu yapo kwenye mechi sita.

Kabla ya kupoteza juzi, ilikuwa imefungwa mechi tatu mfululizo ikianza na Ruvu Shooting, Yanga na KMC na hadi sasa timu hiyo ya jijini Mwanza imekusanya pointi 22 ikiwa nafasi ya 19, huku ikibakiwa na mechi 10, kati ya hizo sita ni za nyumbani.

Mechi hizo za nyumbani ni dhidi ya Coastal, Polisi Tanzania, Lipuli, Mtibwa, Namungo na Ndanda. Itacheza ugenini dhidi ya Prisons, Azam, JKT Tanzania na Simba na rekodi zinaonyesha kuwa ina nafasi ndogo kupata ushindi ugenini.

Ikafanikiwa kushinda ya nyumbani, itakuwa na pointi 40 ambazo kimahesabu zinaweza kuibakiza Ligi Kuu msimu ujao.

Kocha wa timu hiyo, Abdulmutiki Hajji alisema jana kuwa pamoja na matokeo hayo hawajakata tamaa na mkakati wake ni kuhakikisha inashinda michezo sita ya nyumbani, “vijana wanapambana lakini ugenini timu zinaingia uwanjani na matokeo, kwa hiyo hatuwezi kukata tamaa isipokuwa ni kujipanga na sisi kuhakikisha michezo ya nyumbani tunashinda yote.”

Nyota wa zamani wa Yanga, Simba na Taifa Stars, Amir Maftah alisema kwa sasa Mbao kubaki Ligi Kuu itakuwa ni muujiza tu kwani wakati ikipiga hesabu za kushinda nyumbani mechi sita, itapaswa kukesha kwa dua kuziombea timu za juu kupoteza.

Advertisement

“Kwa ujumla hali si nzuri na itakuwa ni muujiza kwa sababu timu nyingi zinapambana kutoshuka Daraja kwahiyo itapaswa kuomba zipoteze yenyewe ishinde, kimsingi wadau waipe sapoti” alisema Maftah.

Let's block ads! (Why?)

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...