Search This Blog

Tuesday, March 10, 2020

Mechi 1,000 za Ronaldo rekodi kama zote

TURIN, ITALIA . KUNA wachezaji wakikupa wasifu wao, lazima unyanyue mkono juu kukubali kuwa wamefanya makubwa sana kwenye soka na mmoja kati ya wachezaji hao ni straika wa Juventus, Cristiano Ronaldo.

Staa huyu juzi kati hapa amefanikiwa kucheza mechi yake ya 1,000 ya kikosi cha kwanza katika ngazi ya klabu na timu ya taifa ya Ureno, huku akiwa amefunga mabao 725 katika mechi hizo.

Kati ya mechi 1,000 alizocheza, mechi 836 ni za ngazi ya klabu na mechi 164 za timu ya taifa ya Ureno, huku mabao 626 akifunga katika ngazi ya klabu na mabao 99 katika timu ya taifa.

Katika maisha yake ya soka kwa Jumla Ronaldo amefanikiwa kutwaa medali kadhaa ikiwemo medali sita za ligi ambazo amezipata katika timu za Manchester United (30), Real Madrid (2) na Juventus (1).

Nahodha huyu wa Ureno, pia ana mataji matano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya aliyoyabeba katika klabu ya Man United (1) na Real Madrid (4), huku pia akiwa na tuzo tano za Ballon d’Or, akizidiwa tuzo moja tu na mpinzani wake mkubwa Lionel Messi mwenye Sita.

Kwa upande wa soka la Kimataifa, Ronaldo amewahi kutwaa taji la Euro 2016 na ubingwa wa UEFA Nations League katika msimu wa 2018–19 akiwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Ureno ambayo yeye ndiye nahodha.

Advertisement

Kuna rekodi kadhaa ambazo Ronaldo anazishikilia katika maisha yake ya soka, moja wapo ni hii ya kuwa mfungaji bora wa muda wote wa Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa na mabao 128 katika mechi 168, alizocheza akiwa Man United, Real Madrid NA Juventus.

Nafasi ya pili katika orodha hii yupo mpinzani wake mkubwa Messi mwenye mabao 114 katika mechi 141.

Ronaldo ndiye mfungaji bora wa muda wote wa Real Madrid akiwa amefunga mabao 311 katika mechi 292, rekodi hii aliweka kwenye kipindi cha miaka tisa aliyokaa Santiago Bernabeu kati ya mwaka 2009 hadi 2018.

Katika maisha yake ya soka Ronaldo amewahi kutwaa mataji yafuatayo, akiwa Sporting Lisboni alibeba taji la Supertaca Candido de Oliveira: 2002, huku alipokuwa Man United akibeba taji la Ligi Kuu England mara tatu 2006–07, 2007–08 na 2008–09.

Kombe la FA mara moja 2003–04, Kombe la Ligi mara mbili 2005–06, 2008–09, Ngao ya Jamii mara moja mwaka 2007, Ligi ya Mabingwa Ulaya mara moja 2007–08, Kombe la Dunia la Klabu mara moja mwaka 2008.

Akiwa Real Madrid, amebeba La Liga mara mbili 2011–12, 2016–17, Kombe la Mfalme mara mbili, 2010–11 na 2013–14, Kombe la Super Cup ya Hispania mara mbili mwaka 2012 na 2017, Ligi ya Mabingwa Ulaya mara nne, 2013–14, 2015–16, 2016–17 na 2017–18, UEFA Super Cup mara mbili 2014 na 2017, Kombe la Dunia la Klabu 2014, 2016 na 2017.

Kwa upande wa Juventus ambako Juzi kati hapa ameweka rekodi ya kufunga mabao katika mechi 11 mfululizo ana taji moja la Serie A 2018–19 na Super Cup ya Italia moja mwak 2018.

Huyu ndiye Ronaldo ambaye katika ushindi wa juzi wa Juventus wa mabao 2-0 dhidi ya Inter Milan alicheza mechi yake ya 1,000 katika ngazi ya klabu na timu ya taifa.

Let's block ads! (Why?)

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...