Search This Blog

Monday, March 23, 2020

Maajabu Kagera, Lipuli yako hapa

By Mwandishi Wetu

Dar es Salaam. Licha ya kutoshika nafasi za juu katika Ligi Kuu Tanzania Bara, Kagera Sugar na Lipuli zimeonyesha safu kali za ushambuliaji.

Wakati Yanga ikionekana kuwa na kikosi bora msimu huu, timu hiyo imezidiwa kwa idadi ya mabao ya kufunga dhidi ya Kagera Sugar, Lipuli na Namungo.

Yanga ambayo iko nafasi ya tatu ikiwa na pointi 51 imeonekana kutokuwa na washambuliaji hodari wa kufunga mabao kama ilivyo Kagera au Lipuli.

Kagera, Lipuli na Namungo hazina wachezaji wa gharama, lakini zimefunga idadi kubwa ya mabao kulinganisha na Yanga kabla ya ligi kusimama kutokana na maambukizi ya virusi vya corona.

Kagera imefunga mabao 36, Lipuli iliyofunga (35) na Namungo (34) ambayo ni zaidi ya Yanga iliyofunga 31.

Pamoja na ubora wa safu zao za ushambuliaji, safu zao za ulinzi zimeruhusu pia idadi kubwa ya mabao ambapo Namungo imefungwa 25, Kagera (31) na Lipuli (39). Singida United imefungwa 49.

Advertisement

Kagera iliyopo nafasi ya nane ikiwa na pointi 41 inaongozwa na kinara wa mabao Yusuf Mhilu aliyefunga 11, Kelvin Sabato (6) na Nassor Kapama (5).

Awesu Awesu (4), Seif Ikobela(3) Peter Mwalyanzi na Geofrey Mwashiuya mawili kila mmoja. Mabao ya Lipuli yamechangiwa na Paul Nonga (11) Daruweshi Saliboko (8), Seif Karihe ( 3), Paul Luyungu, Issa Rashid, David Kamata waliofunga mabao mawili kila mmoja.

Timu ya Namungo yupo Reliants Lusajo aliyefunga 11, Blaise Bigirimana (9) Lucas Kikoti (4), Nzigamasebo Steve (3), Hashim Manyanya na George Makanga mabao mawili kila mmoja.

Akizungumzia kasi ya wazawa msimu huu, kocha wa zamani wa KMC Mrage Kabange alisema nidhamu ya washambuliaji hao imewapa matunda.

“Wamezibeba timu zao wamefunga mabao mazuri ingawa kuna Meddie Kagere naona mengi kafunga kwa penalti, naamini wazawa wana uwezo wa kumfikia,”alisema Kabange.

Kocha wa AFC Arusha, Ulimboka Mwakingwe alisema wazawa wameonyesha wana uwezo wa kushindana na wale wa kigeni.

“Nimevutiwa na washambuliaji wa timu ndogo walivyoweza kuonyesha ubora wao msimu huu. Wanapambana na wageni hicho ndicho kinachotakiwa hii itakuwa na faida kwa klabu zao na timu ya Taifa,”alisema Ulimboka.

Let's block ads! (Why?)

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...