Search This Blog

Friday, March 20, 2020

Lukaku : Ole hakutaka niondoke Man United

Milan, Italia .  KWA mara ya kwanza straika mwili jumba, Romelu Lukaku amefunguka namna kocha wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer alivyojaribu kumzuia asiondoke Old Trafford ikiwa ni misimu miwili tu tangu atue klabuni hapo.
Straika huyo wa kimataifa wa Ubelgiji alijiunga na Manchester United kwa dau la pauni 73 milioni wakati huo Jose Mourinho akiwa kocha wa wababe hao. Hata hivyo, alibadili upepo na kutimkia zake Inter Milan ambayo kwa sasa inanolewa na Antonio Conte.
Lukaku, ambaye mpaka sasa amepachika mabao 23 akiwa na jezi ya Inter Milan, alisema Ole alipambana kuhakikisha anabaki Old Trafford lakini, hakuona sababu ya kuendelea kubaki.
“Kuna msimu unaweza kuwa mbaya na ukabadilisha kila kitu… nilishamaliza kazi pale Man United hivyo, ilikuwa lazima kuondoka,” alisema Lukaku wakati akizungumza na gwiji la Arsenal, Ian Wright kwenye mahojiano yao.
“Nilifanya maamuzi kuwa nakwenda mahali kwngine kwa ajili ya kupata uzoefu na ujuzi mpya katika maisha ya soka….kuna watu walisema kuwa wanataka niende huko,” aliongeza Lukaku.

Let's block ads! (Why?)

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...