Search This Blog

Wednesday, March 11, 2020

Kimenuka...Wawili Kortini kwa kufungua namba zilizofungwa na TCRA



Watu wawili wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka matatu likiwemo la kujihusisha na kufungua Simu zilizofungwa na TCRA ili kubadili uhalisia wa IMEI namba.



Wakisomewa mashtaka hayo na wakili wa serikali Esther Martin mbele ya Hakimu mkazi mwandamizi Augustina Mbando watu hao Abdul Nassor na Said Msangi ambao ni mafundi simu Kariakoo Dar es Salaam wanadaiwa Februari 27 mwaka huu walibadili namba tambulishi ya Simu aina ya Tekno.



Wawili hao pia wanadaiwa kubadili namba za simu tambulishi maarufu IMEI. Ikumbukwe kuwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ilifungia simu zote bandia au ambazo hazikufikia viwango vinavyo takiwa kutumika hapa nchini.

Source Azam Tv


No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...