Search This Blog

Saturday, March 28, 2020

Kagere, Niyonzima wampa maujuzi Gaucho

By Olipa Assa

MSHAMBULIAJI wa Simba Queens,Mwanahamisi Omary amesema  ukaribu wake na Meddie Kagere na Haruna Niyonzima umemfanya kujifunza ufundi kutoka kwao.
Amesema Kagere amekuwa akimshauri kufanya kazi zake bila kuangalia watu wanasema nini kwake huku akimsisitiza kuyafanya mazoezi yawe sehemu ya maisha yake.
"Najifunza mengi kwa Kagere,jamaa ana juhudi binafsi,huwa ananiambiaga umechagua soka kuwa kazi yako litendee haki,kuwa mwanamke wa mfano wa kuigwa wa maendeleo," amesema.
Mwanahamisi amesema Kagere hajaishia kumwambia bali alimpa njumu mpya kama motisha ya kujituma.
Kwa upande wa Haruna Niyonzima wa Yanga, alisema amekuwa akimshauri namna yakuwa mwanasoka bora wa kike.
"Niyonzima ana roho ya kitofauti amewahi kunisaidia pesa kuna kipindi niliumwa,ukiachana na hilo anapenda bidii yangu kwenye soka, Hilo linanipa somo la kujifunza ufundi wao,"amesema.

Let's block ads! (Why?)

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...