Search This Blog

Sunday, March 1, 2020

Iran: Vifo vyaongezeka hadi 54 kutokana na virusi vya corona

Idadi ya vifo vilivyotokana na virusi vya Corona nchini Iran imeongezeka na kufikia 54 kulingana na wizara ya afya, huku pia visa vya maambukizi mapya navyo vikipanda usiku kucha hadi watu 978.

Taarifa ya wizara ya afya imesema maambukizi mapya yamethibitishwa kwenye miji kadhaa ikiwemo Mashhad, ambao ni mji ulio na maeneo matakatifu ya kishia yanayowaleta mahujai kutoka kanda nzima.

Idadi hiyo mpya inawakilisha vifo 11 zaidi ya vilivyoripotiwa Jumamosi na maambukizi makubwa ya watu 385.

Shirika la utangazaji la taifa la Iran limetangaza leo kwamba safari zote za ndege kuelekea jimbo la Gilan zimesitishwa.

Maeneo ya Gilan ndiyo yaliyo na maambukizi mengi baada ya Tehran na mji mtakatifu wa Qom.

 Virusi hivyo vya Corona vilivyoanzia China vimeathiri maafisa saba wa serikali akiwemo makamu wa rais.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...