Search This Blog

Friday, March 6, 2020

Hazard nje miezi miwili

MADRID, HISPANIA . WINGA wa Real Madrid, Eden Hazard amefanyiwa upasuaji wa enka kwa mafanikio jijini Dallas, Marekani, na sasa staa huyo atakaa nje kwa miezi miwili hadi mitatu. Upasuaji huo alifanyiwa na Dkt. Eugene Curry katika hospitali ya The Carrell Clinic.
“Mchezaji wetu Eden Hazard amefanyiwa upasuaji leo (jana), Dallas katika mguu wake wa kulia,” taarifa ya Real Madrid ilisomeka. “Upasuaji huo ulifuatiliwa kwa karibu sana na timu ya madaktari ya Real Madrid.
“Hazard anaendelea kuwa chini ya uangalizi madaktari hadi pale atakaporuhusiwa na kuanza safari ya kurudi kuwa fiti. Atakuwa nje kwa miezi miwili hadi mitatu. Daktari aliyemfanyia upasuaji anafanya kazi na timu ya Dallas Cowboys,
“Curry pia hutibu wanamichezo wadogo na wakubwa ambao hushiriki katika michezo kuanzia kwenye vyuo, shule, wachezaji wa mpira wa kikapu, tenesi, mpira wa miguu wa Marekani, muziki, baseball na michezo mingine mingi.”
Kama utabiri wa madaktari utatimia basi Hazard atarudi uwanjani katika siku za mwisho za msimu huu wa La Liga na pia atakuwa na nafasi ya kushiriki michuano ya Euro 2020.
Mechi ambazo Hazard anaweza kuziwahi, ni ile dhidi ya Leganes, Athletic Bilbao, Alaves, Granada na Villarreal ambazo zote ziko Mei mwaka huu.

Let's block ads! (Why?)

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...