Search This Blog

Saturday, March 7, 2020

Eymael, Sven kitaeleweka Yanga v Simba leo uwanja Taifa

By THOBIAS SEBASTIAN

MAKOCHA na manahodha wa Simba na Yanga wameeleza hisia zao kuelekea mchezo huo wa watani wa jadi utakaochezwa leo Jumapili saa 11:00 jioni kwenye Uwanja wa Taifa.
Kocha wa Yanga, Luc Eymael alisema safari ya kwenda katika mchezo huo hawakuwa na ratiba rahisi kutokana na kila baada ya siku tatu kucheza mechi ambayo ilikuwa inawalazimu kutokufanya mazoezi ya kutosha na wachezaji wengine kuchoka kutokana kutumika sana.
“Nimefurahi kuonana na kocha mwenzangu ambaye tunatoka nchi moja lakini maandalizi ambayo tumeyafanya na wachezaji wangu nina imani watakwenda kuyafanyia kazi ili kupata alama tatu ambazo ndio malengo yetu,” alisema Eymael ambaye ndio mechi yake ya kwanza kukutana na Simba.
Nahodha msaidizi wa Yanga Juma Abdul alisema kwa upande wao wachezaji wamefanya maandalizi ya kutosha yaliyokuwa na mbinu nyingi kulingana na wapinzani wao walivyo na yote hayo ni kuhakikisha wanapata pointi tatu ambazo ndio zitakuwa furaha kwa upande wao.
“Kikubwa kwetu maandalizi tumefanya ya kutosha ili kupata ushindi katika mchezo na Simba ambao tunafahamu ni mgumu na hautakuwa rahisi kwetu kupata ushindi, tunafahamu hilo na tumejipanga nalo ili kukabiliana nao wapinzani,” alisema Abdul.
Kocha wa Simba, Mbelgiji Sven Vandenbroeck alisema wanakwenda kucheza mechi ngumu na kubwa zaidi nchini dhidi ya Yanga na jambo kubwa analotegemea kulioana katika pambano hilo ni ushindani mkubwa kutokana na uimara wa timu zote mbili.
Nahodha wa Simba, John Bocco alisema wanakwenda kucheza mechi ngumu dhidi ya mahasimu wao Yanga, kwani ni timu ambayo ina wachezaji wazuri na kubwa hapa nchini kwa maana hiyo itakuwa ni ushindani wa kila eneo na timu ambayo itafanya maandalizi mazuri ndio itashinda.
Ofisa habari wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF), Cliford Mario Ndimbo alisema; “Kuhusu ujio wa Rais wa CAF, Ahmad Ahmad atapata fursa ya kushuhudia mechi ya Simba dhidi ya Yanga.”

Let's block ads! (Why?)

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...