Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia masuala ya Afya katika Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Dkt Dorothy Gwajima, ameelekeza Manispaa ya Singida kubadilisha kituo cha matibabu kwa ajili ya wagonjwa watakaobainika kuwa na Covid19 (CORONA) kutokana barabara inayoenda huko miundombinu yake kuhitaji marekebisho kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha hivyo kuleta changamoto ya kupitika kwake.
Maelekezo hayo ameyatoa leo katika ziara yake ndani Manispaa ya Singida akikagua matayarisho ya vituo kwa ajili ya kuhudumia wagonjwa husika ikiwemo Kituo cha Afya Sokoine mkoani hapa.
Katika ziara hiyo amebaini Kituo cha Afya Sepuka kilichokuwa kimetengwa kwa Manispaa hiyo miundombinu yake inahitaji kurekebishwa kufuatia mvua kubwa zinazoendelea kunyesha.
Hivyo, Dkt.Gwajima ameagiza mkoa huo utenge eneo mbadala na kutoa taarifa mara moja ndani ya saa 24 ni wapi kituo kitakapokuwa kituo kingine cha kutolea huduma kwa wagonjwa watakao bainika kuwa na ugonjwa huo.
Aidha, Kwa kuongezea Dkt. Gwajima amewataka Waganga Wakuu wote wa Mikoa na Halmashauri kuhakikisha maeneo yote yaliyotengwa yanapitika .
“Wakurugenzi wa Halmashauri hakikisheni maeneo korofi ya barabara yanadhibitiwa kwa kuomba ushirikiano wa TARURA ili kuwezesha shughuli za kijamii kuendelea vyema” ameelekeza Dkt.Gwajima.
Dkt Gwajima amewapongeza watumishi wote wa sekta ya afya, wananchi na wadau wote kwa ujumla kwa jinsi wanavyojitoa katika kuhakikisha nchi inashinda vita dhidi ya Covid19 haraka iwezekavyo.
Search This Blog
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...


No comments:
Post a Comment