Wizara ya Elimu nchini China imesema kuwa chanjo ya virusi vya Corona iliyogunduliwa na taasisi za elimu ya juu nchini humo, itafanyiwa majaribio ya kitabibu au kuanza kutumika haraka iwezekanavyo kuanzia mwishoni mwa mwezi Aprili.
Chanjo hiyo hivi sasa ipo katika majaribio kwa wanyama kwa ajili ya majaribio ya usahihi na ufanisi wake.
Kwa mujibu wa mmoja wa ofisa kutoka Wizara ya Elimu, Lei Chaozi, amesema itaanza kujaribiwa kwa waathirika au kutumika mwishoni mwa mwezi Aprili.
Wizara imevihimiza vyuo vikubwa nchini humo vikiwemo Peking University, Tsinghua University na Xiamen University pamoja na taasisi za utafiti wa kisayansi kuongeza kasi ya utafiti wa chanjo hiyo ili ianze kutumika kwa haraka.
Chanzo: Xinhua News.
Search This Blog
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment