Search This Blog

Wednesday, March 11, 2020

Arsenal bado inamtaka Zaha, Palace yapata mrithi wake

ARSENAL bado inamtaka winga wa Crystal Palace, Wilfried Zaha, Licha ofa zake kadhaa kukataliwa kiangazi mwaka jana. Miamba hiyo ya Emirates haijakata tamaa sasa inajipanga kumnasa staa huyo wa kimataifa wa Ivory Coast.

Habari njema kwa Arsenal ni kuwa tayari Palace inaonekana kukubali yaishe kwa sababu imeshaanza kutafuta mrithi wa winga huyo na jina la staa wa Newcastle United, Allan Saint-Maximin ndilo linalotajwa zaidi kuja kurithi nafasi yake.

Lakini, kama Arsenal haitachangamka inaweza kuzidiwa kete na Bayern Munich inayofukuzia saini ya Zaha pia ambaye msimu huu kiwango chake kimetetereka kidogo kulinganisha na msimu uliopita ambapo alifunga mabao 10 na kupiga pasi 10 za mabao.

Licha ya kupiga pasi za mabao matano na kufunga mabao matatu msimu huu, lakini Arsenal italazimika kuvunja benki kuinasa saini yake maana Crystal Palace inataka dau la Pauni 75 milioni ili kumuachia winga huyo.

Let's block ads! (Why?)

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...