Chama cha ACT- Wazalendo kimeitaka Serikali ya Tanzania kufanya uchambuzi juu ya madhara ya mlipuko wa virusi vya Corona katika uchumi wa nchi na kuwaeleza wananchi namna ambavyo itakabiliana na matokeo hayo.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Halmashauri Kuu ya chama hichokiongozi mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe amewaomba wajumbe kuazimia kutoa maagizo hayo kwa Serikali.
Amesema Serikali haina budi kuchukua tahadhari kwani kulingana na hali ya huduma zetu za kiafya endapo ugonjwa huo utatua nchini utakuwa na athari kubwa kwa Taifa.
“Hakuna Mtanzania ambaye ameripotiwa kuathiriwa na ugonjwa huo lakini virusi vyake vimesambaa nchi nyingi duniani na kuna maelfu ya Watanzania wanakaa China, tuwaombee kwa Mungu ili waendelee kuwa salama,” amesema.
Vilevile, Zitto amesema China ni mshirika mkubwa wa uchumi wa Tanzania katika biashara na uwekezaji na virusi vya Corona vitakuwa na athari katika uchumi hivyo Serikali inapaswa kufanya uchambuzi na kuwaeleza wananchi namna ambavyo itakabiliana na changamoto hizo.
Search This Blog
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment