
LONDON, ENGLAND . STRAIKA wa Chelsea, Tammy Abraham ameshinda tuzo mbili katika hafla ya utoaji wa Tuzo za Soka za Jiji la London, baada ya kubeba tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka wa Ligi Kuu England na ile ya Mchezaji Bora Mdogo wa Mwaka.
Mastaa kibao walikuwepo wakati wa utoaji wa tuzo hizo - David Seaman, Ashley Cole na Carlton Cole walikuwa miongoni mwa magwiji wa soka waliowahi kufanya vizuri katika klabu za London ambao walihudhulia hafla hiyo.
Wakati Abraham akitawala tuzo hizo kwa kunyakua tuzo mbili, kipa wa Watford, Ben Foster alishinda tuzo ya Kipa Bora wa mwaka na straika wa timu ya soka ya wanawake ya Arsenal, Vivianne Miedema alishinda tuzo ya Mchezaji Bora Mwanamke wa Mwaka mara ya pili mfulilizo.
Katika msimu wake wa kwanza katika kikosi cha kwanza cha Chelsea, Abraham, amefunga mabao 15 katika mechi 34 za michuano yote, huku pia akifanikiwa kucheza mechi yake ya kwanza na kufunga bao lake la kwanza kwenye kikosi cha England.
No comments:
Post a Comment