Search This Blog

Tuesday, February 11, 2020

WHO yaonya kuhusu kitisho kikubwa cha virusi vya corona

Shirika la Afya Ulimwenguni - WHO limeonya leo kuwa mripuko wa virusi vya corona ni kitisho kikubwa mno kwa dunia, wakati lilipoandaa kongamano la kwanza kuu kuhusu juhudi za kupambana na janga hilo.

 Karibu wanasayansi 400 wanashiriki katika mkutano huo wa kimataifa mjini Geneva, utakaotathmini jinsi virusi hivyo vinavyoambukizwa na chanzo zinazoweza kupambana navyo.

Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema kuwa wakati asilimia 99 ya visa vya virusi hivyo vinatokea nchini China, bado hali hii inasalia kuwa janga la dharura kwa nchi hiyo, lakini pia na kutoa kitisho kikubwa kwingineko ulimwenguni.

 Virusi hivyo vilivyotambulika kwa mara ya kwanza katika mji wa Wuhan katikati ya Chinba Desemba 31, vimewauwa zaidi ya watu 1,000, kuwaambukiza zaidi ya watu 42,000 na kusambaa katika nchi 25.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...