Search This Blog

Saturday, February 29, 2020

Wanariadha Panga, Magdalena waing'arisha Tanzania Kilimanjaro marathoni

By Imani Makongoro

Dar es Salaam. Wanariadha Joseph Panga na Magdalena Shauri wameitoa kimasomaso Tanzania kwa kutwaa dhahabu katika mbio za Tigo nusu marathoni za mashindano ya Kilimanjaro marathoni yanayoendelea kwenye viwanja vya ushirika mjini Moshi.

Panga ameibuka kidedea upande wa wanaume wakati Magdalena aking'ara upande wa wanawake wakiwapiku wanariadha wengine 5500 waliokimbia mbio  za nusu marathoni.

Tangu mwanzo wa mbio, Panga alikuwa akiongoza akifuatiwa na Watanzania, Josephat Joshua aliyetwaa medali ya fedha, Francis Damiano na Joshua Elisante ambao hata hivyo walipitwa na Mkenya, Joseph Kimathi wa Kenya aliyetwaa medali ya shaba zikiwa zimebakia mita 500 kumaliza mbio.

Kwa wasichana, Magdalena aliibuka kidedea akiwaacha washindani wenzake kwa zaidi ya dakika 5.

Let's block ads! (Why?)

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...