Search This Blog

Friday, February 28, 2020

SERIKALI YA JAPAN YAINGIA MIKATABA MINNE KUUNGA MKONO HUDUMA ZA KIJAMII KATIKA VIJIJI NCHINI TANZANIA


Serikali ya Japan kupitia balozi wake nchini Tanzania Mh. Goto Shinichi Februari 28,2020 jijini Dar es Salaam imeingia mikataba minne tofauti katika muendelezo wa kuendelea kuunga mkono huduma za kijamii katika vijiji mbalimbali nchini Tanzania.

Serikali hiyo ya Japan ikiwakilishwa na Balozi Goto Shinichi imeingia mkataba wa kusambaza magari ya wagonjwa katika hospitali ya KCMC wenye thamani ya dola za Kimarekani 52,996.

Mkataba mwengine ni pamoja na kusaidia mazingira ya elimu katika wilaya ya Meatu mkoani Simiyu wenye thamani ya dollar za Kimarekani 90,729 ikiwa na lengo ya kwenda kuboresha mazingira ya elimu wilayani humo.

Pia serikali ya Japan imeingia mkataba wa ukarabati wa majengo ya shule ya sekondari kizimkazi iliyopo kusini Unguja wenye thamani wa dola za kimarekani 129,596.

Aidha pia serikali hiyo ya Japan imeingia mkataba wa ujenzi wa maktaba ya kujifunzia katika mkoa wa Kilimanjaro wenye thamani ya dola za kimarekani 90,271.



 


No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...