Search This Blog

Friday, February 21, 2020

Saka kamvuruga kabisa Robin van Persie

LONDON, ENGLAND . STAA wa zamani wa Arsenal na Manchester United, Robin van Persie amesema kwamba kila akimtazama Bukayo Saka anawakumbuka mastaa wa nguvu kuwahi kutokea kwenye Ligi Kuu England, Ryan Giggs, Dennis Bergkamp na Paul Scholes baada ya kinda huyo kuonyesha mpira mkubwa sana Arsenal walipojipigia Olympiakos kwenye Europa League juzi Alhamisi usiku.
Saka ameonyesha kiwango bora kwenye mechi kadhaa za Arsenal alizocheza msimu huu na juzi alikuwa staa wa mchezo alipoisaidia timu yake kupata ushindi wa ugenini wa bao 1-0 katika mchezo wa hatua ya 32 bora.
Kinda huyo wa umri wa miaka 18 ndiye aliyetengeneza bao pekee lililofungwa na Alexandre Lacazette dakika tisa kabla ya filimbi ya mwisho baada ya kupiga pasi matata na hivyo kukifanya kikosi hicho cha kocha Mikel Arteta kutoka Ugiriki na kurudi London wakiwa na ushindi muhimu wa ugenini. Hiyo ilikuwa asisti yake ya tisa kwenye michuano yote msimu huu na jambo hilo limemfanya Van Persie amfananishe na magwiji wa Ligi Kuu England.
"Ryan Giggs ndiye aliyekuwa akipiga pasi zile, Dennis Bergkamp, Paul Scholes," alisema straika huyo wa Kidachi.
"Ile ni aina ya pasi inayomtuma straika wake aingie eneo hatari. Ilikuwa ni ya kiwango cha dunia. Safi sana.
"Hii sio rahisi. Hii ilikuwa nzuri sana, kiwango cha dunia. Unaweza kuiona ni rahisi tu, lakini pasi za aina ile, zinapigwa na wachezaji mahiri wanaojua kupiga pasi. Krosi nyingine zimekuwa zikiokolewa na mabeki au zinakuwa juu au chini sana, hazieleweki. Lakini, ile ilikuwa pasi moto. Ile pasi ni ujumbe kwamba ni kitu gani unakitaka kwa washambuliaji wake wafanye."

Let's block ads! (Why?)

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...