Search This Blog

Thursday, February 27, 2020

MWANADIPLOMASIA ASHINDA TAJI LA MISS UTALII PWANI 2020

Prisca Richard Masanja, mwanafunzi wa chuo cha Diplomasia cha Dar es Salaam, ameibuka mshindi wa taji la Miss Utalii mkoa wa Pwani mwaka 2020 ( Miss Tourism Coast Region 2020), katika kinyang'anyilo maalum kilicho fanyika katika hoteli ya kitalii ya Regency Park ,tarehe 26 ,Februari 2020, na kushirikisha jumla ya washiriki 13. 
 
Kwa ushindi huk Prisca Richard Masanja(6), pamoja na washindi wa 2- 5 ,watawakilisha mkia wa pwani katika fainali za kanda za Miss Utalii kanda ya Pwani ya Kaskazini 2020 ( Miss Tourism North Cost Circuit 2020), wakiungana na washindi wa 1- 5 wa mikoa ya Dar es Salaam na Tanga Katika kinyang'anyilo hixho cha Miss Utalii mkoa wa Pwani, ushindani ulikuwa mkali kutokana na washiriki karibu wote kukaribiana kivigezo na sifa. 
 
Elizabeth Samwel Munatta (8) aliibuka mshindi wa pili,huku Lucy Laurent Shirima (1) akiibuka mshindi wa tatu,Mariam Ahmed Kimaro (7) akishika nafasi ya nne,na Jesca Japhet Msechu(5) akiibuka mashindi wa tano. NB:Namba zilizo kwenye mabano ni namba aliyovaa kila mahiriki wakayi wa shindano.


No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...