Search This Blog
Tuesday, February 4, 2020
Mke wa Waziri mkuu wa Lesotho akabiliwa na mashtaka ya mauaji
Mke wa waziri mkuu wa Lesotho Maesaiah Thabane akabiliwa na mashtaka ya mauaji ya mpinzani wake.
Mke huyo wa waziri mkuu anakabiliwa mshtaka ya muaji ya mke wa zamani wa waziri mkuu. Mapema mke huyo wa kwanza Maesaiah Thabane alijiwasilisha mbele ya maafisa wa polisi ili kuhojiwa katika taifa hilo la Afrika ya Kuisni.
Mkewe wa zamani Lipoleo Thabane alipigwa risasi na kufariki nje ya nyumba yake katika mji mkuu wa Maseru siku mbili kabla ya kuapishwa kuwa waziri mkuu 2017.
Shambulio hilo lilidaiwa kutekelezwa na watu wasiojulikana , lakini stakahabadhi zilizowasilishwa mahakamani hivi karibuni na kamishana wa polisi , Holomo Molibeli zimezua maswali chungu nzima.
Agizo la kumkamata Maesaiah Thabane mwenye umri wa miaka 42 lilitolewa mnamo mwezi Januari baada ya kutoweka.
Alikamatwa katika eneo moja la mpakani na Afrika Kusini siku ya Jumanne baada ya makubaliano kati ya mawakili wake na maafisa wa polisi , alisema msemaji wa polisi Mpiti Mopeli akizungumza na chombo cha habari cha AFP.
Kamishna wa polisi Holomo Molibeli aliambia BBC kwamba alikuwa akizuiliwa kizuizini na kwamba atashtakiwa mahakamani siku ya Jumatano.
Watu wengine wanane nchini Lesotho na Afrika Kusini pia wanadaiwa kukabiliwa na mashtaka ya mauaji.
Siku moja tu baada ya waziri mkuu kuhojiwa na polisi, mamia ya mashabiki wa upinzani waliandamana katika mji mkuu wa Maseru wakitaka , ajiuzulu mara moja.
Huku shinikizo kuhusu kesi hiyo ikiendelea , bwana Thabane aliwasilisha ombi la kutaka kujiuzulu , lakini hakutoa tarehe ya kujiuzulu kwake.
Bwana Thabane alielezea mauaji ya mkewe wa zamani 'kama kitendo kichafu' wakati alipotawazwa kuwa waziri mkuu 2017.
Aliandamana katika sherehe hiyo na Maesaiah Thabane.
Kasisi aliwafungisha ndoa wawili hao miezi miwili baadaye katika sherehe iliofanyika katika uwanja wa Maseru.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment