Search This Blog
Wednesday, February 12, 2020
Mfanyabiashara Apigwa Faini mil.9 kwa Kukosa Mashine ya EFD
Mamlaka ya mapato TRA, Mkoa wa Ruvuma imemtoza faini ya shilingi milioni 9 mfanyabiashara anayesambaza pembejeo kwa wakulima kwa kosa la kuuza mbolea bila kutumia mashine ya kutolea risiti ya EFD kama sheria inavyotaka.
Aidha kamanda wa polisi mkoa wa Ruvuma Simon Maigwa amesema jeshi hilo linamshikilia mfanyabiashara huyo kwa kosa la kuuza mbolea kinyume na bei elekezi ambapo urea ilipaswa kuuza kwa shilingi 54,500 lakini yeye anauza kwa shilingi 60,000.
Januari 23 mwaka huu, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme akiwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa huo alifanya ziara kwenye maghala ya kuuzia mbolea kwa lengo la kujua kama wanafuata bei elekezi ya serikali.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment