Search This Blog
Saturday, February 8, 2020
Mbunge wa Babati Vijijini asisitiza Wananchi wakitumie Chuo Cha VETA Manyara
Na John Walter-Babati
Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini Vrajlal Jituson (CCM) amewataka wananchi wa jimbo lake waliokumbwa na Mafuriko na miundo mbinu ya bara bara kuharibiwa, wawe watulivu kwani serikali imeshaanza kuchukua hatua na muda wowote Wakala wa Bara bara vijijini Mijini (TARURA) na Wakala wa Bara bara mkoa wa Manyara (TANROADS) ,watafika katika maeneo hayo yaliyoathiriwa na kuyarejesha katika hali ya kawaida.
Katika hatua nyingine Mheshimiwa Jituson alitoa hamasa kwa wananchi wa jimbo la Babati vijijini katika maeneo ambayo tayari miundombinu ya umeme imefika, kulipia shilingi 27,000 tu ili waunganishiwe huduma hiyo.
Mbunge huyo ameeleza hayo alipokutana na wananchi wa kijiji cha Ufana kata ya Ufana kusikiliza kero mbalimbali zinazowakabili ili zitafutiwe ufumbuzi.
Mpaka sasa Vijiji zaidi ya 140 wilayani Babati vimenufaika na mradi wa umeme vijijini (Rea) ujenzi wa zahanati mpya 18 na vituo vya afya tisa.
Aidha amesema kuwa jimbo hilo amelifanyia mambo mengi katika Nyanja mbalimbali ikiwa ni pamoja na Afya pamoja na Elimu ambapo kwa kushirikiana na Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) wameweza kujenga tawi la Chuo hicho katika eneo la kata ya Ayasanda yenye vijiji viwili vya Endanachan na Ayasanda ambacho kitawawezesha waliohitimu darasa la saba,kidato cha nne na sita kujifunza fani mbalimbali.
Amewataka wananchi wa Babati kutumia vizuri chuo hicho kuwapeleka watoto wao wakapate elimu.
Mkutano huo umekuja baada ya wazee kumuomba diwani wa kata hiyo kumuita Mbunge huyo ili azichukue kero hizo na kuzifikisha kwa wahusika.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...
No comments:
Post a Comment