
MANCHESTER United imeripotiwa inaamini itakamilisha dili la kumnasa Jack Grealish ndani ya mwezi huu kabla ya kufunguliwa kwa dirisha la uhamisho wa majira ya kiangazi mwishoni mwa msimu.
Kiungo huyo mchezeshaji amepewa baraka zote za klabu yake Aston Villa kuhama mwisho wa msimu baada ya kung’ara katika msimu wake wa kwanza kwenye Ligi Kuu England. Grealish amekuwa kwenye kiwango bora licha ya timu yake ya Aston Villa ipo kwenye wakati mgumu wa kupambana kujinusuru isishuke daraja.
Kwa mujibu wa taarifa zilizonaswa kutoka jijini Manchester, miamba hiyo ya Old Trafford inataka kusaini mkataba wa awali mapema kabla ya kufikia kipindi rasmi cha kufanya usajili. Mpango wa Man United ni kukamilisha dili hilo kabla ya Februari hii kumalizika.
Kocha Ole Gunnar Solskjaer amepanga kutumia Pauni 160 milioni kunasa huduma za mastaa wawili wa Kingereza Grealish na James Maddison kwenda kuboresha safu yake ya ushambuliaji. Grealish thamani yake sokoni inatajwa kuwa ni Pauni 80 milioni.
No comments:
Post a Comment