Search This Blog
Wednesday, February 12, 2020
Kocha Luc Eymael alalamikia ratiba ya yanga
PAMOJA na Kocha Mkuu wa Yanga, Luc Eymael, kulalamikia mwenendo wa ratiba, amesema ana uhakika mkubwa wa timu yake kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu kutokana na mabadiliko makubwa yanayoonekana katika kikosi chake.
Akizungumza na Nipashe jijini Dar es Salaam jana, Luc alisema wana ratiba ngumu kwao kwa sababu wanacheza mechi zaidi ya tisa katika mwezi mmoja, hivyo watapambana kuhakikisha wanapata pointi kwenye kila mchezo ili kufikia malengo yao.
Alisema kutokana na ugumu wa ratiba yao na wachezaji kuchoka atahakikisha kikosi chake kitakuwa na mabadiliko ya mara kwa mara lengo likiwa ni kutafuta pointi muhimu ambazo zitawafanya kutwaa taji la ligi hiyo linaloshikiliwa na watani zao, Simba waliopo kileleni wakiwa na alama 53 baada ya mechi 21 ikiwa ni alama 15 zaidi ya Yanga yenye michezo miwili mkononi.
"Licha ya ratiba kuwa changamoto kwetu, kikubwa ambacho nakiona kwenye timu yangu imebadilika kwa kiwango kikubwa na kadiri siku zinavyo kwenda ndiyo inazidi kuwa bora, naamini nafasi ya ubingwa tunayo tena kubwa.
"Hatupaswi kutishwa na anayeongoza ligi, kubwa ni kuendelea kupigana kuona kwanza tunawapita wapinzani wetu ili kuweza kufikia ubingwa kitu ambacho bado kipo kwenye uwezo wetu," alisema huku akilalamika kuwa wachezaji wake si maroboti, kutokana na ugumu wa ratiba ambayo inawafanya kucheza kila baada ya siku tatu.
Yanga ilicheza Alhamisi iliyopita kisha Jumamosi wakacheza tena na juzi Jumanne walicheza na Mbeya City katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam timu hizo kutoka sare ya bao 1-1, sasa itashuka tena dimbani Jumamosi kuikaribisha Tanzania Prisons.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment