Search This Blog

Tuesday, February 4, 2020

Kichuya sasa huru kuitumikia Simba


Klabu ya Simba imethibitisha kupokea Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) ya kiungo, Shiza Kichuya baada ya kuisubiri kwa taribani mwezi mmoja.

Simba imesema kuwa Kichuya sasa anaweza kutumika katika mchezo wowote endapo kocha ataamua kumtumia.

Wachezaji wawili wa Simba, Shiza Kichuya na Luis Miquissone walikuwa wakisubiria ITC zao kwa ajili ya kuanza kuitumikia klabu yao mpya, ambapo hivi sasa Luis Miquissome ndiye aliyesalia kwani hati zake hazijawasili.

"Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) ya Shiza Kichuya imefika. Sasa tupo huru kumtumia kwenye mchezo wowote iwapo kocha mkuu atahataji kumtumia".

Katika taarifa ya klabu, jana Februari 4, ilieleza kuwa ITC ya Miquissome haijawasili ambapo wanahitaji maamuzi ya Kamati ya Hadhi za Wachezaji ya FIFA, baada ya kuitaka Simba ipeleke maelezo ya usajili wake.

Leo, saa 1 Usiku, Simba inashuka dimbani katika Uwanja wa Taifa kucheza na Polisi Tanzania, huku ikiwa kileleni mwa ligi kwa jumla ya pointi 47.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...