Mchezaji Kawhi Leonard ameibuka mshindi wa tuzo ya MVP Kobe Bryant akiiongoza kupata ushindi wa pointi 157- 154 timu yake iliyokuwa chini ya Nahodha LeBron James (Team LeBron) dhidi ya timu ya Giannis Antetokounmpo (Team Giannis)
Kawhi alishinda tuzo hiyo iliyotangazwa na Kamishna wa ligi NBA, Adam Silver tangu Jumamosi kwamba mchezo huo wa All-Star itaitwa kwa jina la Kobe Bryant aliyefariki kwa ajali ya Helkopta mwezi uliopita.
Kawhi aling'ara kwa kufunga pointi 30 na kufunga pointi tatu mara nane kati ya mara 14 alizorusha, anakuwa mchezaji wa kwanza kushinda tuzo hiyo kwa jina la Kobe Bryant huku mwenyewe akimshukuru Bryant kwa mengi aliyowahi kumfanyia kabla na kumpatia tuzo hiyo.
Kawhi alisema,"Hii ina maana kubwa kwangu, maneno hayatoshi kuelezea zaidi ya kumshukuru kwa mengi aliyonifanyia wakati wa mazungumzo yetu na hata kucheza pamoja tuzo hii ni kwa ajili yake".
Katika mchezo huo, timu zote mbili wachezaji walivaa jezi zenye namba 2 kwa timu ya LeBron James na namba 24 kwa timu ya Giannis ambazo alikuwa anavaa Kobe Bryant wakati akicheza ligi hiyo katika misimu yake 20.
Katika mchezo huo uliokuwa una ushindani mkubwa mtupu huru wa mwisho kati ya miwili aliyotupia Anthony Davis "mtoto wa Chicago" ndio ulioamua ushindi kwa timu yake Team LeBron dhidi ya Team Giannis.
Katika sheria mpya iliyotumika kwa mchezo wa All-Star ya msimu huu kwamba mshindi wa mchezo huo atapatikana endapo timu yoyote kati ya hizo mbili itafikisha pointi 157 ambazo ndizo zilikuwa lengo kwa pande zote mbili kuzifikia.
Hapo ndipo mchezo huo wa leo Alfajiri unatajwa kuwa wa ushindani zaidi kwani kila upande ulikuwa unacheza kwa lengo la kufikisha pointi 157 na aliyemaliza mchezo ni Anthony Davis!.
Baada ya Giannis Antetokounmpo kumnyima fursa nzuri mshindani wake LeBron James kwa kuuondoa mpira uliokuwa unaenda kuingia wakati timu yake ikiwa inaongoza kwa 154-153 ilibidi wasubiri hadi mtupo wa Davis.
Wakati timu ya LeBron ikiwa inaongoza kwa tofauti ya pointi moja pekee (156-155) ndipo Anthony Davis alipochezewa faulo na kupata fursa ya kupiga mitupo huru (miwili) kwa timu yake ikimaanisha katika mitupo hiyo alitakiwa kufunga mmojawapo ili kuipa ushindi timu yake.
Hata hivyo Davis ambaye ni mzaliwa wa Chicago ulipochezwa mchezo huo, alikosa mtupo wa kwanza na kuzua hofu kwa timu yake na mashabiki wa timu hiyo kabla ya kufanikiwa kufunga kwenye mtupo wa pili na kuipa ushindi uliofikia lengo la kufikisha pointi 157 ili kushinda mchezo huo.
Ni katika robo ya mwisho ya mchezo huo upinzani zaidi kama wengi wanavyotamani iwe kila msimu pale ambapo timu ya Giannis ilikuwa na nafasi nzuri ya kuibuka na ushindi ingefunga pointi 24 ikiwa inaongoza kwa pointi 133 dhidi ya zile 124 za timu ya LeBron na ingezifikia pointi lengwa 157 kutokana na pointi 24 za robo ya mwisho zilizowekwa kumuenzi Kobe Bryant kutokana na namba aliyokuwa kwenye kila kipindi cha pili cha kucheza kwake ligi hiyo hadi anastaafu.
Ukiachana na Dola Laki moja kwa kila timu ilizokuwa inashinda kupelekwa kusaidia mifuko mbalimbali ikiwemo shule zilizopo Chicago kama ilivyochanguliwa na LeBron na Giannis, timu ya LeBron ulishinda jumla ya Dola laki nne baada ya mchezo kwa ujumla ikiwa ni ushindi wa robo ya kwanza (Dola laki moja) na Dola Laki tatu za ushindi wa mchezo huo.
No comments:
Post a Comment