Search This Blog
Tuesday, February 11, 2020
Hekari 750 za ardhi kurejeshwa Kigamboni
Rais John Magufuli ametoa muda wa siku Saba kwa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kurudisha umiliki wa ardhi yenye ukubwa wa hekari 750 kwa manispaa ya Kigamboni mkoani Dar es salaam kuwa chini ya manispaa hiyo na si wizara.
Rais Magufuli ametangaza uamuzi huo wakati akizindua rasmi wilaya ya Kigamboni mkoani Dar es salaam, ambapo pia amezindua majengo mbalimbali yatakayotumika kama ofisi wilayani humo.
Amesema kuwa, hatua hiyo itasababisha halmashauri hiyo ya Kigamboni kutumia eneo hilo la ardhi kwa shughuli mbalimbali za kijamii.
Wakati wa uzinduzi huo Rais Magufuli pia ameiagiza Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kutafuta Shilingi Bilioni Mbili kwa ajili ya kujenga nyumba za Watumishi wa wilaya ya Kigamboni na nyumba hizo zijengwe ndani ya kipindi cha miezi Sita.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...
No comments:
Post a Comment