Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres amesema upo uhusiano kati ya mabadiliko ya hali ya hewa na nzige waliovamia nchini Ethiopia na katika eneo la Afrika Mashariki.
Guterres ameyasema hayo mjini Addis Ababa kabla ya mkutano wa kilele wa nchi za Umoja wa Afrika unaoanza hii leo.
Mada kuu ya mkutano huo wa 33 ni usalama. Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema uvamizi wa wadudu hao ni mbaya zaidi kuwahi kutokea Afrika Mashariki mnamo kipindi cha miaka 25.
Ameelezea wasiwasi wake kwamba uvamizi huo unaweza kusababisha baa la njaa katika nchi ambazo tayari zinapambana na ukosefu wa chakula.
Nchi zilizoathirika kutokana na uvamizi wa nzige ni Ethiopia, Somalia, Kenya, Eritrea na Sudan huku kukiwa na kitisho cha wadudu hao kuenea hadi Uganda na Sudan Kusini.
Kuhusu mkutano, Guterres amesema anaamini kwamba ukosefu wa utulivu katika eneo la Sahel na nchini Libya utapatiwa ufumbuzi na kwamba Umoja wa Mataifa unaziunga mkono juhudi za nchi za Afrika.
Search This Blog
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment