
MANCHESTER, ENGLAND . KOCHA, Pep Guardiola amesema furaha ndicho kitu kutakachomfanya afanye uamuzi kama wakuendelea kubaki Manchester City zaidi ya msimu ujao.
Mhispaniola huyo ana msimu mmoja zaidi kwenye mkataba wake wa sasa kabla ya kufika mwisho na jambo hilo litamfanya awe kwenye benchi la Man City kwa miaka mitano.
Lakini, adhabu ya kufungiwa misimu miwili kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya kumeibua utata mkubwa kama Guardiola atasaini mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia timu hiyo baada ya huu wa sasa kufika mwisho.
Licha ya Guardiola mwenyewe kusisitiza kwamba atabaki Etihad hadi mwisho wa mkataba wake, lakini kama Man City itashindwa kwenye rufaa yake ya kupinga kufungiwa misimu miwili kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, suala la kubaki kwenye kikosi hicho kwa muda mrefu bado kuna utata mkubwa.
Alipoulizwa kama atabaki Etihad baada ya msimu ujao kumalizika, Guardiola alisema: “Sifahamu. Nataka kubaki mwaka mmoja zaidi na baada ya hapo itategemea. Naangalia furaha yangu, hicho ndicho kitu ninachokitaka. Kila mtu anahitaji furaha.
“Hiyo ndiyo sababu kubwa, ninapoamua kuonndoka, basi ni kwa sababu nafikiria furaha yangu kwamba ninakokwenda nitafurahi kuliko ninapotoka.
“Tutalizungumza hilo mwisho wa msimu au katikati ya msimu ujao. Kitu muhimu ni kwamba sijutii hata sekunde uamuzi wa kuja hapa na kuongeza mkataba wangu. Baada ya hilo, matokeo nndicho kitu kinachoshikilia ajira zetu. Kila kocha anafukuzwa, kila kocha ana matatizo, kila kocha ana nyakati nzuri na mbaya, huo ndio ukweli na mimi sina tofauti.”
Man City ya Guardiola Jumatano ijayo itashuka uwanjanni kukipiga na Real Madrid kwenye mchakamchaka wa Ligi ya Mabingwa Ulaya mchezo wa mtoano wa hatua ya 16 bora.
No comments:
Post a Comment