Search This Blog

Monday, February 3, 2020

Dereva bodaboda ampa mimba mtoto wa darasa la 3

Mtoto mwenye umri wa miaka 13 ambaye alikuwa akisoma katika Shule ya Msingi Msakila Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi, amekatishwa masomo yake akiwa darasa la 3 kwa kupewa ujauzito ambao sasa una miezi saba na mtu aliyefahamika kwa jina la Salum Mayunga dereva bodaboda.

Akizungumza kwa masikitiko makubwa mtoto huyo amesema kuwa, wazazi wake wote wawili walifariki na kuchukuliwa na ndugu ambao walimwambia aende akaishi na kijana huyo, bila kujali ni mwanafunzi na pia umri wake ni mdogo.

Consolata Mlaponi ni mmoja kati ya watu waliojitolea kumsaidia mtoto huyo ambapo amesema kuwa kwa sasa mtoto huyo anakabiliwa na hali ngumu ya kimaisha, ikilinganishwa na umri wake ambao ni mdogo na hawezi kujitafutia.

Huku Jeshi la Polisi mkoani humo likianzisha oparesheni kabambe yenye lengo la kuwabaini na kuwakamata wale wote wanaojihusisha na vitendo hivyo.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...