Search This Blog

Friday, February 28, 2020

Birdman Amaliza Bifu na Watoto Wake Lil Wayne, Drake na Nick Minaj



BAADA ya bosi wa Cash Money Bryan, Williums Birdman kusumbuana kwa muda mrefu na rapa Lil Wayne, bosi huyo amefunguka kuwa kwa sasa wako poa sana na wanazungumza vizuri.

Wawili hao wametajwa kuwa katika bifu zito tangu mwaka 2015 ambapo Wayne alisema kuwa anamdai Birdman na Cash Money Record zaidi ya dola milioni 50 ambazo ni zaidi ya bilioni 115 za madafu kama fidia baada ya lebo hiyo kuvunja mkataba na kuichelewesha album yake ya Carter V.

Akizungumza katika kipindi cha Dj Akademiks, Birdman aliweka wazi mahusiano yake na Wayne pamoja na wasanii wengine aliofanya nao kazi Cash Money kama Nick Minaj na Drake na kudai kuwa kwa sasa wamemaliza tofauti zao na hawana tatizo.
“Ni kweli nimekuwa katika mgogoro na mtoto wangu Lil Wayne, lakini kwa sasa tumeshazimaliza tofauti zetu na tunazungumza sana, lakini pia nina mahusiano mazuri na Drake na kila siku ninamtazama Nick Minaj kama mdogo wangu wa kike,” alisema Birdman.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...