
DAVID Beckham amekamilisha bonge la dili katika klabu yake ya Inter Miami baada ya kufanikiwa kunasa saini ya straika wa Paris Saint Germain, Neymar, ambaye amekubali kutua kwenye klabu hiyo ya Ligi Kuu Marekani miaka 10 ijayo.
Wakati Barcelona na Real Madrid zikipambana kuisaka saini yake, Mbrazil huyo amefanya makubaliano na Beckham ambaye ni mmiliki wa Inter Miami kuwa atajiunga na timu hiyo kabla ya kustaafu.
Dili lenyewe lilikuwa hiv, wawili hao walikuwa wamekaa wakipiga stori huku tukio hilo likirushwa moja kwa moja na Cheneli ya YouTube, OTRO, ndipo Beckham alipompa Neymar karatasi isiyo na kitu na kumtaka asaini iwe kama makubaliano kutua Inter miaka 10 ijayo.
Licha ya Beckham kumwambia Neymar timu yake hailipi pesa ndefu, lakini alikubali.
No comments:
Post a Comment