Search This Blog

Friday, January 31, 2020

Zidane kanuna kisa Pogba

MADRID, HISPANIA.KISEMWACHO ni kwamba Kocha wa Real Madrid, Zinedine Zidane huenda akasusa na kuitema timu hiyo baada ya rais wa klabu, Florentino Perez kushindwa kumletea kikosini kiungo, Paul Pogba, inaelezwa.
Kocha Zidane, ambaye awali yake ya kwanza aliyofanya kazi Bernabeu akiwa kocha alibeba mataji matatu mfululizo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, anahaha kunasa huduma ya staa huyo Mfaransa mwenzake kutoka Manchester United.
Dili la Pogba limekwama baada ya Man United kugomea ofa iliyohusisha kubadilishana wachezaji James Rodriguez na Mariano Diaz.
Kwa mujibu wa Soccerlink, jambo hilo linamfanya Zidane kufikiria kuachana na Real Madrid mwishoni mwa msimu. Kinachompa wasiwasi zaidi Zidane ni kwamba anaona kabisa Pogba anaweza kumtikia zake Juventus, alikowahi kuwa huko nyuma.
Perez hakutaka kusajili mchezaji mwingine wa pesa nyingi baada ya kumnasa Eden Hazard kwa karibu Pauni 100 milioni katika dirisha lililopita la majira ya kiangazi. Kwenye dirisha hilo, Madrid iliwanasa pia Eder Militao, Ferland Mendy, Luka Jovic na Rodrygo.
Kama Madrid itashindwa kabisa kumsajili Pogba, badi ripoti zinadai kwamba Zidane anaweza kushawishika kuhitimisha maisha yake Bernabeu na kutimkia kwingineko. Mpango wa Madrid kwa sasa ni kubeba La Liga na Ligi ya Mabingwa Ulaya ambapo kwenye hatua ya mtoano ya 16 bora wamepangwa kukabiliana na Manchester City.

Let's block ads! (Why?)

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...