Search This Blog

Tuesday, January 14, 2020

YANGA YASAJILI MSHAMBULIAJI MGHANA

 klabu ya Yanga Sc imetangaza usajili wa mchezaji raia wa Ghana, Bernard Morrison mwenye umri wa miaka  26, kutoka klabu ya DC Motema Pembe ya nchini DRC Congo.

Takwimu za Morrison: Ligi kuu Afrika Kusini amecheza michezo 18 na kufunga mabao mawili, ligi kuu Ghana katika michezo 16 ametikisa nyavu mara 6.

Mchezaji huyo anamudu kucheza nafasi mbalimbali uwanjani katika safu ya ushambuliaji, mshambuliaji wa kati na mshambuliaji wa pembeni akitokea kulia ama kushoto.

Bernard amewahi kuchezea timu kadhaa kabla ya kutua Jangwani katika dirisha hili dogo la usajili, amepita As Vita, Dc Motema Pembe, Ashanti ya Ghana na Orlando Pirates ya Afrika Kusini.

Imeandikwa na @abasi_shabani_17


No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...