Juhudi za uokozi bado zinaendelea katika mji wa Elazig kufuatia tetemeko la ardhi la kipimo cha Richter 6.8, lilopiga mashariki mwa Uturuki.
Watu wapatao 29 wamepoteza maisha huku wengine kadhaa wakiwa bado wamekwama chini ya vifusi vya majumba yaliyoporomoka, hayo ni kulingana na taarifa ya Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uturuki Suleyman Soylu.
Waziri huyo ameongeza kwamba zaidi ya watu 15,000 wamekimbilia kwenye vituo vya muda vya kuwahifadhi watu ikiwa ni pamoja na kumbi za michezo na za vyuo vikuu. Watu wengine 5,000 wamejihifadhi katika mahema.
Wengine wapatao 1,500 wamepelekwa hospitalini kwa matibabu huko mjini Elazig pamoja na miji mingine jirani.
Kitovu cha tetemeko hilo kilikuwa ni wilaya ya Sivrice ya Elazig, lakini pia lilitikisa maeneo ya miji mengine ya karibu.
Search This Blog
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment