Ukraine imetangaza leo kuwa itazilipa fidia ya dola 8,000 za Marekani familia za raia wake waliokufa kwenye ajali ya ndege iliyotokea Iran mapema wiki hii.
Mpango huo umetangazwa na rais wa Ukraine Volodomyr Zelensky ambaye amesema pia atalazimisha Iran kutoa kiwango kingine cha fedha kitakacholipwa kama fidia kwa familia za wahanga.
Watu 176 wakiwemo raia 11 wa Ukraine walikufa wakati ndege ya shrika la Ukriane chapa Boeing 737 ilipoanguka muda mfupi baada ya kuruka kutoka uwanja wa ndege mjini Tehran.
Hapo jana maafisa wa Iran walikiri ndege hiyo ilianguka baada ya kushambuliwa kwa bahati mbaya na kombora la jeshi la Iran.
Rais Zelensky alizungumza kwa njia ya simu na rais Hassan Rouhani wa Iran ambaye ameahidi nchi yake itawafungulia mashtaka wote waliosababisha kutokea ajali hiyo.
Search This Blog
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment