Ujumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Malawi (MEC) leo (Jumatatu) umefanya ziara ya kikazi kwenye ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa lengo la kubadilishana uzoefu juu ya mambo mbalimbali yanayohusu uendeshaji wa chaguzi.
Ujumbe huo wa watu 11 ambao umeongozwa na Mwenyekiti wa MEC Jaji Dkt. Jane Ansah umekutana na kufanya mazungumzo na Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuhusumasuala mbalimbali yanayohusu usimamizi wa uchaguzi katika nchi hizi mbili.
Akizungumza katika kikao cha pamoja baina ya Tume hizo mbili, Mwenyekiti wa NEC Jaji Rufaa (Mst.) Semistocles Kaijage ameonyesha kufurahishwa kwake kwa Tume ya Uchaguzi ya Malawi kuitembelea NEC ili kubadilishana uzoefu.
Amesema.“Tanzania na Malawi ni wanachama wa umoja wa Tume za Uchaguzi wa nchi za SADC ambao mojawapo ya malengo yake ni kujengeana uwezo katika kusimamia chaguzi. Nafurahi kuona mmechagua kuja Tanzania ili kujifunza na kubadilishana uzoefu”
Naye Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Malawi Jaji Dkt. Jane Ansah ameishukuru NEC kwa kufanikisha kikao hicho cha pamoja kwani masuala mengi ya msingi yameweza kujadiliwa.
Amesema “mazungumzo haya yameibua masuala mengi ya msingi kwa pande zote mbili. Sisi tunaondoka hapa tukiwa na uelewa mpana zaidi wa masuala haya yahusuyo usimamizi wa chaguzi hasa taratibu za ugawaji wa majimbo ya uchaguzi”.
Ujumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Malawi unajumuisha Mwenyekiti wa Tume, Makamishna 5, Mkurugenzi wa Uchaguzi na Maofisa wengine 4.
Search This Blog
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment