Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli amesema Serikali zote mbili ya Mapinduzi ya Zanzibar na ya Muungano itashirikiana kwa pamoja kuwaunga mkono wawekezaji ili nchi ipate maendeleo.
Hayo ameyasema huko katika Hoteli ya Verde Mtoni wakati wa ufunguzi wa Hotel hiyo ikiwa ni miongoni mwa shamra shamra za kuadhimisha miaka 56 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ambayo yamemkomboa Mzanzibar.
Alisema wawekezaji wanaowekeza katika visiwa hivi kwa sababu ya amani na utulivu ulikuwepo jambo ambalo linawapa imani ya kuekeza na kujipatia Maendeleo nchini .
Pia alisema Mapinduzi ya 1964 ilikuwa na lengo la kuuondowa utawala dhalimu wa Kisultani kwa kujipatia uhuru wa nchi na kuweza kujiongoza wenyewe kwa kujipatia maendeleo mbali mbali kupitia miradi ya ikujenga ustawi wa nchi .
Aidha alimpongeza mmiliki wa hoteli hiyo kwa kuwekeza kwani kufanya hivyo kutaweza kupatikana fursa za kufikia watalii wengi na kuzidisha pato kwa Serikali pamoja na vijana kujipatia ajira .
Hata Hivyo alisema fursa ziko nyingi Zanzibar na amewataka wawekezaji waendelee kuwekeza mbali ya kukuza utalii , zipo fursa nyengine kama kilimo na uvuvi na mambo mengine ya maendeleo.
Vile vile alisema wawekezaji ambao wanaoekeza ni vyema kutoka ndani ya nchi yao sio kutoka nje ya nchi na serikali inaahidi kutoa mashirikiano, ijapokuwa wanaviazio vidogo vya mtaji wao .
“wawekezaji sio watoke nchi za nje bali wajitokeze wa ndani ya nchi na Serikali itawapa mashirikiano, wala wasikate tamaa, kwani hata Mwekezaji huyu alianzia chini hadi sasa yuko juu”,alisema Magufuli.
Nae Waziri wa Fedha na Mipango Mohamed Ramia Abdilwawa amesema hoteli hiyo imejengwa kwa uzalendo na inaonyesha njia ya kujipatia maendeleo katika Nyanja mbali mbali za kuingiza pato kwa Serikali.
Pia amempongeza muwekezaji huyo kwa kulipa kodi kwa wakati na kuwaomba wawekezaji wengine wawe na tabia kama hiyo kwani kulipa kodi kwa wakati kunaengeza pato la Serikali .
Amesema wawekezaji wazalendo wanapata fursa ya kuwekeza na kuzidisha uchumi wa Nchi, hayo ndio malengo ya Mapinduzi Matukufu katika kuimarisha maendeleo.
Kwa upande wake Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bakhressa Group of Companies Salim Azizi Salim akitoa maelezo mafupi ya hoteli kutoka kwa mmiliki wa mradi amesema hotel hiyo imejengwa ya kisasa na ina kila aina ya kuvutia kwa watalii ikiwemo sehemu za kuogelea na ina vyumba 106.
Pia alisema fursa nyingi zimetoka za ajira ambapo zaidi ya nafasi 250 zimetolewa kwa wananchi na wameweka sehemu nyingi za vivutio kiwemo sehemu za watoto za kusherehekea sikukuu.
Mmiliki huyo alimpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein kwa uongozi wake wa busara katika nchi na kuendeleza yale mazuri yote ya Mapinduzi yaliyoanzishwa tokea mwaka 1964.
Search This Blog
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment