Search This Blog
Thursday, January 23, 2020
PADRI Aliyefungasha Ndoa ya Stamina Afunguka "Wasije Wakaanzisha Mahusiano Mengine Kwani Watatenda Dhambi"
PADRI wa Kanisa Katoliki, Dk Bernard Msike ambaye aliwafungisha ndoa staa wa Hip Hop, Bonaventure Kabogo ‘Stamina’ na mkewe Veronica Peter katika Kanisa la Mt. Maria Consolata mkoani Morogoro, amewaita wanandoa hao kanisani kwa ajili ya usuluhishi.
Padri huyo aliwafungisha ndoa hiyo Mei, 2018 ambayo imedumu kwa takriban mwaka mmoja na miezi kadhaa kisha kumwagana na kuzua gumzo kama lote mitandaoni wiki iliyopita.
Padri huyo alisema atawaita wawili hao kanisani kwa ajili ya usuluhishi kwani kanisa bado linaitambua ndoa yao. “Niwaase tu katika kipindi hiki wasije wakaanzisha mahusiano mapya maana watakuwa wanatenda dhambi. Kanisa Katoliki linaitambua ndoa ya mwanaume na mwanamke mmoja tu mpaka kifo kitakapowatenganisha,” alisema.
Stamina na mkewe wameachana na mkali huyo kutoa wimbo wa Asiwaze ambao unatajwa kuwa amemsema mkewe huyo. Sababu kubwa inayotajwa katika kuachana kwa wawili hao ni usaliti
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment