
Paris, Ufaransa. ACHANA na mzuka ambao mashabiki wa mpira wa kikapu jijini Paris waliupata wakati waliposogezewa mchezo wa Ligi Kuu ya Kikapu Marekani (NBA) ikiwa ni mara ya kwanza kufanyika huko.
Mchezo huo ulizikutanisha Milwaukee Bucks na Charlotte Hornets ambapo nyota wa Bucks Giannis Antetokounmpo alikiwasha vilivyo akifunga pointi 30 kwenye ushindi wa 116-103. Hata hivyo, burudani zaidi ilinoga wakati mastaa wa Paris Saint-Germain wakiongozwa na Neymar Jr na Kylian Mbappe walipovamia kushughudia mtanange huo.
Neymar na Mbappe waliongozana na mastaa wengine wa PSG kina Marquinhos, Mauro Icardi, Marco Verratti na Thiago Silva na kuufanya ukumbi wa AccorHotels Arena kunoga zaidi.
Kama kawaida Neymar alikuwa na jezi ya chama lake Charlotte Hornets yenye jina na namba yake anayotumia pale PSG na timu ya Taifa Brazil. Mastaa wenzake walikuwa wamevalia majaketi na fulana zenye nembo ya klabu ambapo walipigwa picha wakiwa wamekaa eneo moja.
No comments:
Post a Comment