Search This Blog
Wednesday, January 8, 2020
Naibu Waziri Nditiye aagiza TCRA Kukagua mabasi yote yanayosafirisha vifurushi bila kuwa na leseni
Na Ezekiel Mtonyole, Dodoma.
Naibu Waziri wa Ujenzi uchukuzi na mawasiliano, Mhandisi. Atashasta Nditiye, ameitaka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA, kuhakikisha wanasimamia na kukagua mabasi yote yanayo safirisha vipeto, bahasha na vifurushi bila ya kuwa na leseni kutoka Mamlaka hiyo na kuwataka wanaofanya hivyo kuacha Mara moja.
Nditiye ametoa maagizo hayo leo januari 8, 2020 Jijini Dodoma wakati akifungua mkutano wa 26 wa Baraza la wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania, waliokutana kutathmini na kuweka mipango mipya ya kuimarisha Shirika hilo.
Nditiye amesema licha maagizo yake ya awali, lakini bado mpaka Sasa Kuna mabasi ya abiria yanasafirisha vipeto bila ya kuwa na leseni na kutaka TCRA kufanya ukaguzi wa kina kuhakikisha wanayabaini mabasi hayo na kuyachukulia hatua Kali za kisheria.
"Nataka nitoe maagizo TCRA mkafanye msako licha ya maagizo niliyotoa lakini bado Kuna mabasi bado yanasafirisha vipeto, bahasha na vifurushi wakafanye msako kuhakikisha mabasi yote yanayosafirisha yanakuwa na leseni, na yafuate taratibu zote za kusafirisha vifurushi hivyo" amesema Naibu Waziri Nditiye.
Amesema lazima Shirika la Posta waendelee kuimarisha huduma zao na kutoa huduma bora kwani Kuna baadhi ya mizigo ni Siri na nyingine ni Mali za Serikali na lazima zisafirishwe na shirika hilo na si vinginevyo na shirika ndilo lenye uwezo wa kusafirisha mizigo vizuri.
Aidha amefurahishwa na utendaji kazi mzuri wa Shirika hilo hali iliyopelekea Shirika hilo kuondolewa miongoni mwa mashirika yaliyo katika hatari kuondolewa huku akiwataka watumishi hao kujiamini na kusema wanapoona wanakwazwa na vitu wasisite kutoa taarifa.
Pia amemtaka Posta Masta Mkuu wa Shirika la Posta kuhakikisha wanafungua ofisi za kubadilisha fedha katika miji yote mikuu na kuweka watu maalumu na kuhakikisha hazifungwi kwa wakati wote.
"Siku si nyingi nilikuwa na dola nikataka kubadilisha nimeenda ofisi zote nikakuta zimefungwa nikashangaa na ofisi za Posta nazo zimefungwa, Sasa nataka mkafungue ofisi kwenye miji yote mikubwa na kuhakikisha hazifungwi" amesema.
Kwa upande wake Posta Masta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Hassan Mwang'ombe, amesema mkutano huo ni wa mwaka na huwakutanisha Mameneja wa Mikoa na watumishi wa makao makuu wanaokutana kujadili utendaji kazi na kupanga mipango mipya ya mwaka ya Shirika hilo, ambapo pia amesema wamejipanga na wameanzisha huduma kwa njia ya Mtandao kuboresha huduma hiyo.
Huku kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Kitolina Kippa amesema licha ya kazi kubwa zinazofanywa na shirika hilo bado kunachangamoto katika kwa baadhi ya Wilaya kutokuwa na ofisi za Posta.
Wakati inaelezwa kuwa Kuna ofisi za Posta 158 lakini Kuna baadhi ya Wilaya zikiwa hazina Ofisi za Posta Kama Wilaya ya Nyang'wale ikiwa ni miongoni mwa Wilaya zisizokuwa na Ofisi za Posta.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment