Search This Blog

Thursday, January 2, 2020

Mwakinyo apigia hesabu ubingwa dunia

By Imani Makongoro

Dar es Salaam. Baada ya kuporomoka kwa nafasi tatu kwenye viwango vya ngumi duniani, Hassan Mwakinyo amesema atatumia pambano lake la  mwezi ujao la ubingwa wa dunia kurudi katika ubora wa kimataifa.
Mwakinyo ameporomoka kutoka nafasi ya 17 hadi ya 20 kwenye viwango vya ngumi za kulipwa duniani katika uzani wa super welter vinavyotolewa na mtandao wa ngumi wa dunia (boxrec).
Bondia huyo wa nyota nne licha ya kuendea kuwa namba moja Afrika katika uzani wa super welter, ameporomoka katika ubora wa dunia huku akieleza sababu ni kutopigana mara kwa mara.
“Mabondia wa nyota tano, nne na nusu mpaka nne kama mimi wako wengi na wanapigana mara kwa mara, wakishinda wanaongeza pointi na kupanda,”alisema Mwakinyo.
Bondia huyo ambaye pambano lake la mwisho alimchapa kwa pointi Arnel Tinampay wa Philippines  Novemba, mwaka jana alisema ana matarajio ya kupanda mara zaidi kwenye viwango hivyo mwezi Februari. “Nitacheza pambano la ubingwa wa dunia, naamini litanipandisha mara dufu katika ubora,” alisema bondia huyo namba moja nchini.
Alisema ameanza maandalizi ya pambano hilo ambalo litaadaliwa na promota wake Ally Mwanzoa akiamini atashinda na litamuongezea nyota zaidi kutokana na maandalizi anayofanya.
Naye bondia Salum Mtango ambaye anatokea katika kambi yake, Mwakinyo alisema anatarajia ubingwa utabaki nchini.

Let's block ads! (Why?)

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...